Mahakama ya kimataifa ya ICC imetoa onyo kali kwa wanablogu nchini Kenya,wanaotoa taarifa kuhusu mashahidi waliofika mbele ya mahakama ya ICC.
Hii ni baada ya taarifa kuhusu shahidi wa kwanza mbele ya mahakama hiyo kujitokeza kwenye mitandao hasa kwenye blogu, twitter na Facebook kumhuusu.
Blogu hiyo ya udaku pia ilichapisha picha ya mwanamke huyo
Baadhi ya taarifa zilisema kuwa amewahi kutoa ushahidi wake ambao haukutofautiana na alikiambia mahakamy ya ICC, katika mahakama nchini Kenya lakini ukapuuziliwa mbali na mahakama.
Mashahidi hao wanatoa ushahidi wao ndani ya mahakama ila wamefichwa nyuso zao hatua iliyochukuliwa ili kuwalinda kutokana na tisho lolote dhidi ya maisha yao.
ICC huenda ikachukua hatua za kisheria dhidi ya wanaosambaza taarifa kuhusu mashahidi wanaofika mbele ya mahakama hiyo.
Jaji anayeongoza vikao hivyo, Chile Eboe-Osuji, alisema kuwa ni makosa kisheria kuwafichua mashahidi wakati mahakama imebana kuwatambulisha.
Shahidi huyo ambaye wenye blogu wanasema wanamfahamu, ni mwanamke mwathiriwa wa shambulizi dhidi ya Kanisa la Kiambaa ambako yeye na wanakijiji wenzake walitafuta hifadhi wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi kutokota katika mkoa wa Rift Valley.
Watu zaidi ya thelathini waliteketezwa wakiwa hai ndani ya kanisa hilo
*************************************************
original post at BBC SWAHILI